Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule (katikati) akizungumza jambo leo Septemba 26, 2024 wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa na Kinondoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna bora ya utekelezaji wa majukumu bila kujihusisha na vitendo vya rushwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam. (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondon.
Mkuu wa Ushirikishwaji wa jamii Wilaya ya Kinondoni ASP Elina Maro akizungumza jambo wakati akichangika mada katika warsha ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.
Msaidizi wa Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni INSP Christopher Mwambona akizungumza jambo wakati akichangika mada katika warsha ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni .
Mkuu wa Idara ya Tathimini na Ufatiliaji WAJIKI Bw. Hancy Obote Mahenge akizungumza jambo wakati akichangika mada katika warsha ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni
Mkuu wa Dawati la Uelimishaji Umma Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa na Kinondoni Dorothea Mrema akizungumza jambo wakati akitoa elimu katika warsha ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni
Afisa Habari wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni Gillian akifatilia mada mbalimbali katika warsha ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.
Afisa wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni Ismail Mwayungu akitoa ufafanuzi wa jambo katika warsha ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni wakiwa katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa na Kinondoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee, Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge wakiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto limetakiwa kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha katika vyombo vya mahakama watu wote wanaobainika wanafanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto katika jamii.
Akizungumza leo Septemba 26, 2024 wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa na Kinondoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni iliyofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule, amesema kuwa zipo jitihada mbalimbali zinazofanywa na madawati ya kijinsi jambo ambalo limesaidia watuhumiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Shida ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wakinama bado ipo, hivyo tunakazi ya kufanya ikiwemo kukumbushana majukumu yetu na kulichukulia jambo hili kwa uzito mkubwa” amesema Mhe. Mtambule.
Mhe. Mtambule amesema kuwa madhara ya ukatili wa kijinsia ni mkubwa kwa mtoto, hivyo ni jukumu kwa kila kiongozi kusimamia sheria bila kuingia katika vishawishi wa aina yoyote ikiwemo kupokea rushwa.
Amewataka maskari kusimama imara na kuendelea kuwatetea watoto pamoja na kutojiingiza katika vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee, amesema kuwa warsha hiyo itawasaidia maafisa wa madawati ya kijinsia kaika kubadili mtazamo wa jamii kwa kutatua changamoto zilizopo.
Amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji na uwazi katika mchakato wa kutoa huduma jambo ambalo litapunguza mianya ya kupokea na kutoa rushwa.
“Maafisa wa madawati mkasimamie sheria, kanuni na utaratibu katika kutimiza uwajibu wenu ili kulinda taswira ya serikali pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii” amesema Nyakizee.
Naye Msaidizi wa Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kipolisi Kinondoni INSP Christopher Mwambona ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kutoa taarifa za kuwafichua watuhumiwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsi ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua.