Dar es Salaam, Septemba 25, 2024
Airtel Tanzania imezindua kampeni kabambe ya ‘JiBoost na Airtel Money,’ inayotoa unafuu kwa watumiaji wake kwa kuwapatia bonasi ya shilingi 20,000 kwa kila muamala wanaoufanya. Kampeni hii inalenga kuboresha maisha ya kila siku ya wateja kwa kuwazawadia pesa wanapotumia huduma za Airtel Money kwa miamala mbalimbali.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, alisema, “Tunataka wateja wetu wahisi thamani ya kutumia Airtel Money katika maisha yao ya kila siku, iwe kwa kununua muda wa maongezi, intaneti, au kufanya malipo ya huduma za serikali kama LUKU. Kampeni ya ‘JiBoost’ inalenga kuwapa nafasi ya kufurahia bonasi kupitia miamala wanayoifanya kila siku.”
Diamond Platnumz, Balozi wa Airtel Tanzania, aliisifu kampeni hii kwa kutoa fursa kwa watumiaji kurejeshewa fedha kwa kila muamala wanaoufanya. “Hii ni nafasi ya kuokoa na kupata pesa zaidi huku ukiendelea na shughuli zako za kila siku,” alisema Diamond.
Kwa upande wake, Joti, maarufu kama Mr Money, alibainisha kuwa kampeni ya JiBoost ni njia ya kuleta furaha kwa watumiaji kwa kuwarudishia sehemu ya pesa wanazotumia kwenye malipo mbalimbali kama vile umeme, TV, na ununuzi wa vifurushi.
Wateja wa Airtel Money wanaweza kufurahia bonasi hizi kwa kutumia App ya MyAirtel au kupiga *150*60#, na kwa kila muamala, watapata ujumbe wa kuthibitisha bonasi hadi shilingi 20,000.