Na WAF, MPWAPWA
Wanachi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wameshindwa kuzuia hisia zao mara baada ya kupokea huduma za kibingwa kutoka kwa Madaktari bingwa wa Rais Samia walioweka kambi ya siku sita wilayani humo.
Wakizungumza Septemba 25, 2024 hospitalini hapo wamesema wengi wao waliokwama kumaliza changamoto za kiafya kwasababu za kiuchumi kwa ajili ya kuzifuata huduma hizo mbali yapata km. 107 hadi Dodoma mjini.
Gabriel Magubike mkazi wa Mpwapwa amesema ujuo wa Madaktari Bingwa umewapunguzia safari ya kufuata huduma mjini kama Hospitali ya mkoa au Benjamini Mkapa.
“Nilipopatiwa huduma nilishauriwa kwenda Benjamin Mkapa Hospitali lakini nilienda kama mara mbili nikashindwa hivyo tunamshukuru Rais kutuona watu wa chini”, amesema Bwa Magubike.
Naye Basiliana Mdachi mkazi wa Mpwapwa Madukani ambaye amekiri kuzunguka kwa muda mrefu bila mafanikio amesema ujio wa Madaktari hao umemuwezesha kupata suluhu ya tatizo lililomtesa kwa zaidi ya miaka minne.
Akizungumza Hospitalini hapo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mpwapwa Dkt. Hamza Mkingule amekiri kuwepo kwa ongezeko la wananchi kuchangamkia huduma hizo za kibingwa.
“Ndani hizi siku mbili za huduma tumewasajili takribani ni wananchi 300 wamefika kupata huduma hivyo wanaimani kabisa hadi mwisho wa kambi kufikisha wananchi wasiopungua 1200” amesema Dkt. Mkingule na kuongeza kuwa,
“Kila Daktari Bingwa tumempatia watu wawili ambao anawajengea uwezo ili mwisho wa kambi wawe wameturithisha ujuzi”, amesisitiza Dkt.Mkingule.
Wilaya ya Mpwapwa imepokea jumla ya Madaktari Bingwa wa wanane wakiwepo wa Watoto, Wanawake na Uzazi, Meno na Kinywa, Mifupa, Magonjwa ya ndani pamoja na Uwepo wa Muuguzi Mbebezi kwa ajili ya huduma watakazo zitoa kwa siku sita wilayani humo.