Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa bandari mpya ya Mbamba Bay katika Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma tarehe 25 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Barabara mpya ya kiwango cha lami ya Mbinga – Mbamba Bay yenye urefu wa kilomita 66 katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma tarehe 25 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Nyasa mara baada ya uwekeaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Bandari mpya ya Mbamba Bay na ufunguzi wa Barabara mpya ya kiwango cha lami ya Mbinga – Mbamba Bay yenye urefu wa kilomita 66 katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma tarehe 25 Septemba, 2024.