Picha ya pamoja kati ya waandishi wa habari na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) katikati ni Naibu waziri wa Katiba na Sheria, Jumnne Sagini aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa akifungua semina na ziara kwa Waandishi wahabari juu ya shughuli na kazi zinazofanywa na JICA na Ubalozi wa wa Japani nchini.
*************
Na James Salvatory
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) limetoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini ili kuwajengea uelewa juu shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo.
Mafunzo Hayo ya siku tatu, yanaenda sambamba na ziara katika miradi inayotekelezwa JICA katika mkoa wa Dodoma katika wilaya mbalimbali ikiwemo Kondoa.
Akifungua Mafunzo hayo Mkoani Dodoma Mapema leo, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa amesema kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari kufahamu kwa kina shughuli mbalimbali za JICA na Ubalozi wa Japani nchini Tanzania na kuujulisha umma kwa usahihi.
Katika ziara hiyo, waandishi wa habari wametembelea mradi wa Ukarabati visima katika kijiji cha zuzu ambapo Vijiji 4250 vimepata maji safi (GRASSROOTS) ikiwa japan imesaidia kurekebisha kisima na sasa wanakijiji wame ufaika.
Mradi mwingine ni wa sekta ya barabara II (RSSP II) ambapo umefadhiliwa na benki ya Maendeleo ya afrika AFDB kupitia mfuko wa maendeleo ya Afrika ADF, Shirika la maendeleo la kimataifa la Japan JICA na serikali ya Tanzania kwa jumla ya gharama ya Dola za Marekani milioni 212.78 kwa ajili ya kujenga barabara ya Dodoma (manyamanya)-babati(Boga ).
Miradi mingine ni O&OD iliboreshwa na kufanikisha Vijiji kubadilika kwa kasi, mwingine Miradi / shughuli za Japan /Jica oda ambapo utafiti wa biashara kuunga mkono Tengeneza Ajira na Ongeza kipato wa tano ni wa kuboresha uwezo wa usimamizi wa Hospitali za Rufaa (RRHMP) na wa Mwisho ni Program ya kujitolea (JOCV).
Katika hatua nyingine Balozi Yasushi Misawa amewataka watanzania kuwa watu wa kuzingatia muda wakati wakifanya majukumu yao ya kila siku ili kuokoa muda unaoweza kupotea pasipo sababu za msingi Hali ambayo inachangia kurudisha nyuma uchumi wa nchini.
“Huwa nashangaa rafiki zangu wa kitanzania wakipoteza muda hata hawakasiriki kabisa na hawajali jambo ambalo kwa kwetu Japan tunazingatia muda ” alisema Balozi
Kwa upande wake Afisa utawala na Mawasiliano JICA Tanzania, Alfred Zacharia, amesema uwepo wa miradi ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan litasaidia kuboresha mahusiano ya kijamii na kiutamaduni.
Picha ya Pamoja kati ya Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa na Mwakilishi Mkuu wa JICA, Ara Hitoshi, katika ni Naibu waziri wa Katiba na Sheria, Jumnne Sagini.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa na Naibu waziri wa Katiba na Sheria, Jumnne Sagini wakifurahia jambo pamoja.
Picha mbalimbali za Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa na Mwakilishi Mkuu wa JICA, Ara Hitoshi, wakiwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ,Jumanne Sagini .
Mshauri wa Uchumi baina ya Japani na Tanzania Christopher Ntaigiri akitoa wasilisho lake mbele ya Waandishi wa habari mkoani Dodoma.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiendelea kusikiliza ma wasilisho yalitolewa kwenye semina hiyo iliyofanyika mkoani Dodoma.