Na Ashrack Miraji (Fullshangwe Media), Tanga
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Japhari Kubecha, amemkabidhi kiti mwendo (wheelchair) Bi. Ester, mkazi wa Magomeni, Tanga, ambaye amekuwa akihangaika kutembea kwenda kwenye shughuli zake za kiuchumi.
“Awali ya yote, nitoe shukrani za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuguswa na tukio hili la dada yetu Ester, ambaye hivi karibuni alionekana mitandaoni akitembea kwa shida huku akiomba msaada kutoka kwa watu mbalimbali,” alisema Kubecha.
Aliendelea kwa kueleza kuwa, baada ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, kuona video hiyo, alimwagiza kumsaidia Ester kwa niaba ya Rais. “Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempa dada Ester kiti mwendo ambacho kitamwezesha kufanya shughuli zake kwa ufasaha zaidi,” aliongeza.
Mhe. Kubecha pia alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Tanga kumshirikiana na Mhe. Rais kwa kazi kubwa anazozifanya kwa ajili ya taifa. “Leo tunaona namna ambavyo Mhe. Rais anavyowajali wananchi kupitia taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali. Niwaombe tushirikiane naye katika kazi hizi kubwa kwa manufaa ya taifa letu,” alihitimisha.