Meneja wa Bank of Africa Tanzania Tawi la Arusha Bw.Francis Mizambwa, akimkabidhi zawadi ya simu mshindi wa droo ya tatu ya kampeni ya kidijitali ya BOA Bw.Innocent Boniphace Kisole katika hafla fupi iliyofanyika tawi la Arusha .
BANK OF AFRICA-TANZANIA iliendesha droo yake ya mwisho ya bahati nasibu ya kampeni yake ya kidijitali “Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15 Pro” ambapo , Bw. Inocent Boniphace Kisole mteja wa benki hiyo aliibuka mshindi wa zawadi ya I-phone 15 Pro. Bahati nasibu hiyo ilifanyika katika ofisi kuu ya BANK OF AFRICA, mbele ya Mkaguzi Mwandamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bi. Irene Kawili. Kampeni ya Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15 Pro ilianza tarehe 11 Juni 2024 na imedumu kwa miezi 3.
Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo, Mratibu wa Bidhaa na huduma za kidijitali wa BANK OF AFRICA, Bw.Fortunatus Joachim alisema “ wakati kampeni inaelekea ukingoni tunafurahishwa na ushirikishwaji na msisimko ambao kampeni hiyo imeleta kwa wateja wetu ambayo mafanikio yake yameonekana mazuri kupitia ukuaji wa mapato”.
Naye Mkuu wa Mawasiliano na Masoko na Mawasiliano Bi. Nandi Mwiyombella aliongeza kuwa benki hiyo inatarajia kuendelea na kampeni na shughuli shirikishi zaidi zitakazopelekea mwingiliano zaidi wa bidhaa na huduma za benki hiyo na zawadi za kusisimua zitatolewa.
Kampeni hii ni kielelezo cha lengo la kimkakati la Benki kuweka bidhaa na huduma zake katika mfumo wa kidijitali na hivyo kukuza ushirikishwaji wa kifedha pamoja na urahisi wa wateja kupata huduma za benki.