WANAFUNZI ya Skuli mbalimbali wa Unguja na Pemba wakifuatilia sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Elimu Bila Malipo Zanzibar, yaliyoadhimishwa katika Uwanja wa New Amaan Complex Jijini Zanzibar leo 23-9-2024.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Skuli za Msingi wa Unguja na Pemba wakishiriki katika Halaiki ya kuadhimisha Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Elimu Bila Malipo Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Jijini Zanzibar leo 23-9-2024.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wageni waalikwa na Wakuu wa Idara za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Elimu Bila Malipo Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar leo 23-9-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Elimu Bila Malipo Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Jijini Zanzibar leo 23-9-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Kombe la Nidhamu Afisa Elimu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mohammed Shamte, Mkoa huo kuibuka msindi wa nidhamu kwa mwaka huu 2024, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Elimu Bila Malipo Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Jijini Zanzibar leo 23-9-2024, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Mohammed Mussa na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa.(Picha na Ikulu)