Freeman Mbowe, amekamatwa leo Jumatatu, Septemba 23, 2024, wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari katika eneo la Magomeni, Dar es Salaam ambapo alikuwa akinajiandaa kushiriki maamdamano ambayo chama hicho kiliyaanda Leo Septemba 23, 2024.
Tukio hili linakuja baada ya tangazo la Freeman Mbowe la tarehe 11 Septemba 2024, ambapo alitangaza maandamano ya kulaani ongezeko la matukio ya utekaji na mauaji ya watu wasio na hatia, ikiwemo tukio la hivi karibuni la kutekwa na kuuawa kwa Ali Kibao, aliyekuwa kada wa Chadema.
Mbowe aliweka wazi kwamba maandamano hayo yalikuwa ni sauti ya wananchi waliochoshwa na vitendo vya ukatili na ukosefu wa haki, na alisisitiza kuwa hawatasita kuendelea kushinikiza uwajibikaji kutoka kwa viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama, ikiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni.
Jeshi la Polisi, kupitia msemaji wake David Misime, lilijibu kwa kuyapiga marufuku maandamano hayo na kurejerea kwenye mazungumzo badala ya maamdamano hatua ambayo imeleta hisia tofauti katika jamii.