Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa wakati wa kikao cha wafanyakazi
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai akielezea kuhusu maendeleo ya maandalizi kikao cha CardioTan kinachoandaliwa na Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joachim Asenga akijibu hoja za wafanyakazi wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Thadei Kavishe akielezea miundombinu mipya ya maabara inayowekezwa itakavyopunguza muda wa wagonjwa kusubiria majibu kwa muda mrefu wakati
wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akielezea namna kitengo hicho kimejipanga kuendelea kufanya tafiti mbalimbali wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
………….
Na: Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupeleka huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo katika maeneo mbalimbali nchini kwa kufungua kliniki za matibabu kuwapunguzia wagonjwa adha ya kufuata huduma hizo Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa kikao na wafanyakazi wa taasisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa vikao hivyo vinavyofanyika kila baada ya miezi mitatu.
Dkt. Kisenge alisema JKCI imeanza kufungua kliniki za kutoa huduma za matibabu ya moyo katika mkoa wa Geita Hospitali ya Chato na mkoani Arusha kupitia hospitali iliyopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
“Tumekuwa tukipokea wagonjwa kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao wanafika JKCI wakiwa wamechoka, kupitia kliniki zetu za Geita na Arusha wagonjwa waliopo kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa watapata urahisi wa kufika na kupata huduma kwa wakati”, alisema Dkt. Kisenge
Aidha Dkt. Kisenge alisema JKCI imefanya maboresho ya miundombinu kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wanaotibiwa lakini pia kuifanya hospitali hiyo kuendelea kuwa taasisi bora Afrika Mashariki na Kati.
“Katika maboresho tunayoyafanya tumeweza kuongeza vyumba vya watu mashuhuli (VIP wards) kutoka vyumba 10 hadi 17 kutokana na uhitaji wa vyumba hivyo kuwa mkubwa”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake Afisa Muuguzi wa JKCI Paulo Josephat aliupongeza uongozi wa Taasisi hiyo kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi yanayoongeza motisha wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Paulo alisema maslahi ya wafanyakazi yamekiwezesha Kitengo cha Utafiti na Mafunzo kuendelea kutoa tafiti bora zinazoielimisha jamii kuhusu magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo.
“Kitengo cha Utafiti na Mafunzo kinafanya kazi nzuri sana kupitia tafiti wanazotoa pamoja na kutafuta fedha kutoka kwa wahisani kwaajili ya wagonjwa wanaotibiwa JKCI wasiokuwa na uwezo wa kulipia matibabu”, alisema Paulo
Naye Afisa Ubora wa Huduma wa JKCI Hildergard Karau aliwakumbusha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kuvaa vitambulisho wanapokuwa kazini pamoja na kufuata miongozo ya kazi.
Hilda alisema mfanyakazi anapovaa kitambulisho eneo la kazi kinamsaidia mgonjwa kuwafahamu watoa huduma wa Taasisi pale mgonjwa anapohitaji kupata huduma ama maelezo kutoka kwa mtoa huduma.