Wekundu wa Msimbazi Simba Sc imefanikiwa kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Al-Ahli Tripol katika mchezo wa marudiano hatua ya 32 bora uliopigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
Haukuwa ushundi mwepesi kwa Simba Sc kwani walilazimika kutoka nyuma baada ya kutanguliwa Ahli kufunga goli kupitia mshambuliaji wa Kimataifa wa Angola Agostinho Cristovao Paciencia ‘Mabululu’ dakika ya 17.
Mshambuliaji wa Simba Sc Kibu Dennis Prosper alianza kuifungia simba bao la kusawazisha kwa tik-tak dakika ya 36 kabla ya mshambuliaji Christian Leonel Ateba Mbida kufunga bao la pili dakika ya 45 + 1, huku mzawa Edwin Charles Balua akafunga bao la tatu dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo Simba Sc hatua ya 16 bora ambayo uchezwa kwa makundi kufatia sare ya bila mabao kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Tripoli