RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Pwani Benki ya CRDB Ndg.Idd Badru, akitembelea banda la maonesho la Benki ya CRDB, wakati wa ufunguzi wa Tamasha Pili la “Fahari ya Zanzibar” linalofanyika katika viwanja vya Maonesho Dimani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 20-9-2024, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe.Shariff Ali Shariff.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg.Arafat Ally Haji,akitembelea banda la maonesho la Benki ya PBZ, wakati wa ufunguzi wa Tamasha Pili la “Fahari ya Zanzibar” linalofanyika katika viwanja vya Maonesho Dimani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 20-9-2024, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe.Shariff Ali Shariff na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) Juma Burhani .(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea Maonesho ya Tamasha la Pili la “Fahari ya Zanzibar” alilolifungua leo 20-9-2024, katika viwanja vya Maonesho Dimani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Mhe. Hamida Mussa Khamis na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Shariff Ali Shariff.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Tigo Zantel Zanzibar Ndg.Azizi Said Ali, wakati akitembelea maonesho ya Tamasha la Pili la “Fahari ya Zanzibar” linalofanyika katika viwanja vya Maonesho Dimani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 20-9-2024, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Shariff Ali Sharii, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA Ndg. Juma Burhan.(Picha na Ikulu)