Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillius Wambura wakati aliposhiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moshi Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 17 Septemba 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali kabla ya kufunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakati kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 17 Septemba, 2024.
………………
RAIS wa Jamhuri ya Muungano na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema hayupo tayari kuona amani na utulivu nchini inavurugika au inapotea kwa sababu ambazo hazina msingi ikiwemo vikao vilivyopangwa kwa ajili ya kufanya vurugu kwa lengo ya kuiondoa madarakani serikali yake.
Rais Samia aliyasema hayo leo katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi (TPS), koani Kilimanjaro.
“Nataka niwaambie vikao vyote vitakavyokwenda kupanga uovu, uovu mnaopangwa tutaupata kumepangwa sijui kumepangwa kushusha moto hadi Samia aseme basi naondoka,
“Hiyo Serikali au Serikali ya Samaki? Hiyo ni serikali ya samaki ndugu zangu Maanake Samaki kila akiwa mkubwa na akili inafanyaje? Hiyo ni akili ya samaki lakini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiondoshwi hivyo.”
“Sasa kwa kutumia kofia ya Amiri Jeshi Mkuu katika nchi hii niseme kwamba tumeapa kuilinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano.
“Na kwamba tutafanya kila linalowezekana kuimarisha ulinzi wa maisha na uhai wa maisha ya Watanzania kwa kuwa ni jukumu letu.
Aidha, Rais Dk. Samia alisema alizisikiza clip za wanasia wa waili ambazo zilionesha wote wakitoa taswira ya mipango ya uvunjifu wa amani inayopangwa na baadhi ya vyama vya siasa.
“Na yaunganisha haya na maamuzi kikao chaSeptemba 11mwaka huu kilichofanyika au kilichofanywa na chama kimoja cha siasa kile Ngulelo mkoani Arusha.
“Kikao ambacho kimeadhimia kuwatumia na kuwachochea vijana kwa kuzusha tuhuma dhidi ya jeshi la polisi, kufanya siasa chonganishi kwenye misiba na kushusha morali kwa jeshi la polisi ili washindwe kufanyakazi yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
“Lakini nashukuru kwenye kikao hicho hicho, mkutano ulibaini na ulitambua kwamba nchi hii ya Tanzania ina intelejensia kubwa na kwamba walipeana onyo wanapofanya mipango yao miovu watumie vyema fursa walioipata kwenye R4.
“Lakini nawashukuru waetambua kuwa nchi hii ina telejensia kubwa na ushahidi ni kwamba yote yaliyosemwa kule mimi ninayo huo ndio ubora wa intelejensia yetu.
“Niliwahi kusema na hapa nataka nirudie tena kwa msisitizo, ukimya wangu sio ujinga na wala kuzungumza sana kwa wale wanaozungumza sana sio werevu hata kidogo, kuzungumza sana ni debe tupu tu haliachi kuvuma lazima litavuma kwahiyo ukimya wangu sio ujinga na kuropokwa kwao sio werevu.
“Mliponikabidhi dhamana hii niliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na dhamana yangu pamoja na Vyombo vya Ulinzi ni kulinda amani ya Nchi yetu kwahiyo sitokuwa na muhali na yoyote anayetaka kuvuruga amani hiyo ya Nchi yetu, tumevumiliana kwenye mengi lakini kwenye kulinda Tunu ya amani na utulivu ya Nchi, nirudie tena sitokuwa na muhali na yoyote anayeratibu, anayeshiriki hata anayetekeleza mipango hiyo miovu,”alisema Rais Dkt. Samia