Katika mitaa ya Sinza jijini Dar es Salaam , hasa pale Mwenge Afrika Sana, kuna jina linalotambulika kwa wengi Mwafrika Merinyo.
Mwanamume huyu maarufu, mwenye kofia yake ya kipekee, amekuwa kielelezo cha heshima na utambulisho katika sanaa na mitindo kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Kwa jina lingine, Merinyo anafahamika pia kama “Mzee Afrika Sana”, jina lililopewa eneo hilo kutokana na umaarufu wake. Ikiwa umewahi kutembelea Afrika Sana, basi huwezi kumsahau huyu mpokeaji wa “BIMA YA PENZI”.
Mbali na umaarufu wake katika eneo hilo, Mwafrika Merinyo ni gwiji wa uandishi. Ameandika vitabu maarufu kama “Kifo cha AIDS” na “Watoto wa Mjini”, ambavyo vilichapishwa katika miaka ya 1980.
Vitabu hivi vilichochea mijadala mikali kuhusu changamoto za kijamii, afya na maisha ya watoto waliokosa malezi sahihi mjini.
Hivi sasa, Mzee Afrika Sana ameamua kuweka silaha zake chini na kusalimisha moyo wake kwa “BIMA YA PENZI”. Hii ni hatua ya kipekee inayowakumbusha watu juu ya umuhimu wa kulinda mapenzi yao na kuyathamini.
Kwa hiyo, unangoja nini kupata “BIMA YA PENZI” yako?
Kwa wale wanaotaka kujiunga na harakati hizi, unakaribishwa kutembelea maduka ya vitabu kupata nakala yako ya vitabu vya Merinyo. Vinginevyo, unaweza kupiga simu namba 0713 864 229 kwa maelezo zaidi.
Sisi tunasisitiza jambo letu moja: UNAPENZIKA, UNA BIMA?