Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiwasili katika eneo la mradi wa kuchakata taka kwa ajili ya mbolea ya asili uliopo Mabwepande Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo Septemba 13, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiwakatika ziara ya kutembelea na kukagua eneo la mradi wa kuchakata taka kwa ajili ya mbolea ya asili uliopo Mabwepande Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo Septemba 13, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akita maelekezo wakati wa ziara katika eneo la mradi wa kuchakata taka kwa ajili ya mbolea ya asili uliopo Mabwepande Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo Septemba 13, 2024.
Shughuli za uchakataji wa taka zikiendelea katika eneo la mradi wa kuchakata taka kwa ajili ya mbolea ya asili uliopo Mabwepande Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo Septemba 13, 2024.
……………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea na kukagua mradi wa kuchakata taka kwa ajili ya mbolea ya asili uliopo Mabwepwande katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar
es Salaam leo Septemba 13, 2024.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, amesema mradi huo utasaidia kutunza mazingira kwani jamii itapata nafasi ya kukusanya taka na kuzielekeza katika kiwanda hicho na kuepusha zisizagae ovyo.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Kijaji ameitaka Manispaa ya Kinondoni inayoendesha mradi huo kushirikiana na wadau wa sekta binafsi katika uendeshaji wa kiwanda hicho.
Waziri Dkt. Kijaji amewataka kuwatengenezea miundombinu wananchi kutengenganisha taka wanapozipeleka kwenye mradi huo kwa ajili ya kuchakatwa na kuwa mbolea
Amesema kushirikiana na wadau hao kutasaidia kuongeza ufanisi wa kazi ya kukusanya taka na kwamba eneo hilo la kiwanda ni kubwa na bado halijapata kutumika inavyotakiwa.
Waziri Dkt. Kijaji ameielekeza manispaa hiyo kuboresha mazingira ya eneo hilo la ukusanyaji wa taka kwa ajili ya kuchakatwa na kuwa mbolea ya asili ili kuwa rafiki kwa wafanyakazi.
Sanjari na hilo, pia ameelekeza kuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho kupatiwa vifaa (mask) vya kujikinga na hewa inayotokana na taka zinazikusanywa hapo ili kulinda afya zao.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme ametoa wito wa kupanua wigo wa mradi huo iwe ni kukusanya taka nyingi zaidi na kuzalisha bidhaa zingine Zaidi ya mbolea.
Amesema zinahitaji taka nyingi ziwe ni mali badala ya kuishia zaidi kwenye madampo kwani uzalishaji wa taka jijini ni mkubwa kuliko zinazopelekwa kwenye mradi huo.
Amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua mradi wa kuchakata taka kwa ajiliya mbolea ya asili uliopo Mabwepwande katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo Septemba 13, 2024.
Mradi wa mbolea ya asili unatekelezwa kwa ufadhili wa Jiji la Hamburg la nchini Ujerumani lililoingia makubaliano na Serikali ya Tanzania kwa kiasi cha shilingi Zaidi ya bilioni 4.
Katika ziara hiyo Waziri Kijaji ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Mndeme, Mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Ufuatailiaji wa Kaboni (NCMC) Prof. Eliakim Zahabu na Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Kanizio
Manyika.