Na Mwandishi wetu, Mirerani
Wanafunzi 168 wa darasa la saba wa shule ya msingi Jitegemee kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro mkoani Manyara wamemshukuru Mungu baada ya kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi hivyo kuwa na matarajio ya kuendelea na elimu ya sekondari.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Jitegemee, Godwin Mollel amesema wanafunzi hao 168 wamefanya mitihani yao salama na wana matumaini ya kufaulu na kuanza kidato cha kwanza mwaka 2025.
Mwalimu Mollel amesema wanafunzi hao wamemweleza kuwa mitihani yao haikuwa migumu na wamefanya kwa umakini wakitarajia kufaulu.
“Haikuwa kazi nyepesi hadi kufika hapa hivyo tunamshukuru Mungu kwa yote na wanafunzi wangu wanajiamini na wamenihakikishia ,” amesema mwalimu Mollel.
Amewapongeza wanafunzi hao kwa kuhitimu elimu ya darasa la saba na hivi sasa wanajipanga ili wafanye mahafali ya kumaliza darasa la saba.
Mmoja kati ya wanafunzi wa shule ya msingi Jitegemee aliyefanya mtihani huo Elia Msafiri amesema anamshukuru Mungu wanafunzi wote wamemaliza salama mtihani na wanatarajia kufaulu.
“Tunamshukuru Mungu tumemaliza salama na matarajio yetu tutafaulu wote kwa kudura za Mungu kwani mtihani haukuwa mgumu sana hivyo tunatarajia ufaulu,” amesema.
Mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani Amina Said amesema anamshukuru Mungu kwa hatua hiyo kwani wamefanya mitihani ya kuhitimu na kumaliza salama.
“Tunatarajia kufaulu wanafunzi wote kwani wenzangu walikuwa watulivu na tumefanya mitihani yetu kwa umakini mkubwa na tunatarajia ufaulu mkubwa,” amesema