MTANDAO wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania umeazimia kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuzungumzia hatma ya masuala ya utekaji na ukatili yanayoendelea nchini pamoja na kumkumbusha mikataba ya kimataifa ya kupinga ukiukwaji wa haki za binadàmu.
Amesema wadau wa haki za binadamu wamekuwa na changamoto kubwa katika kupambana na utekaji, mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu na hivyo wameomba kukutana na Rais Samia ili kuona namna ya kupata suluhu ya kukabiliana na changamoto hizo zinazogharimu maisha ya watu.
“Tulitoa mapendekezo yetu kwa Rais Samia kuhusu uundaji wa tume rasmi ya kiraia ya kudumu inayohusisha watu wengi na tulimshauri aridhie mikataba miwili ya kimataifa inayopinga masuala ya utekaji na ukatili na ndio maana leo tumeadhimia kwenda kukutana naye baada ya miaka mitatu kupita “
Amesema mkutano huo wenye ajenda ya Kuboresha namna ya kupata Rasilimali za ndani,unalenga kumshawishi Rais aridhie kusaini mikataba miwili ya kimataifa inayopinga masuala ya ukatili nchini.
Mtendaji Mkuu wa (TPSF), Raphael Maganga ambaye alikuwa mgenirasmi amesema jukumu kubwa la sekta binafsi ni kuona namna inayoweza kushirikiana na taasisi mbalimbali kukuza utetezi wao katika haki za binadamu.
Maganga amesisitiza kuwa sekta binafsi zina wajibu wa kutetea haki za binadamu kama watoto,vijana na wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa uhuru na ufanisi zaidi.
Amesema taasisi za kutetea haki za binadamu zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa ila zinapaswa kuwa imara na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi ili kuhakikisha jamii yote inakuwa na haki sawa.