Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba akifunga kongamano hilo leo Mkoani Arusha .
…….
Happy Lazaro, Arusha .
Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba amezitaka nchi za Afrika Mashariki kuendelea kuimarisha Mfumo wa kieletroniki wa ununuzi wa umma (NEST) ili kuleta thamani halisi ya fedha kwenye miradi inayotekelezwa kwa lengo la kuleta manufaa kwa jamii.
Dkt Mwigulu ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akifunga Kongamano la 16 la ununuzi wa umma la Afrika Mashariki na uzinduzi wa mfumo wa kieletroniki wa ununuzi wa umma (NeST) .
Aidha amezitaka taasisi za umma kutumia fursa hiyo kuinua uchumi wa Afrika Mashariki kwa kutengeneza mikakati ya kuendelea katika mashirikiano katika nchi Jumuiya za Afrika Mashariki..
“Kutokana na umuhimu huo, tayari nimemuelekeza Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, ahakikishe anaratibu jambo hili na kulisimamia kwa karibu ili Sera na Mkakati huo vianze kutumika mapema iwezekanavyo,Kwa kufanya hivyo, tutaweza kuweka utaratibu mzuri zaidi wa kusimamia fedha zinazotengwa kwa ajili ya ununuzi wa umma na ugavi kila mwaka.”amesema.
Aidha amesema kuwa,mifumo irahisishe kazi ya Manunuzi na kuharakisha Maendeleo ambapo amesema Sheria ni moja inayotungwa kuongoza taasisi hizo za Manunuzi hivyo anatarajia kuwa watafanya kazi kwa ufanisi zaidi hususani katika Matumizi ya mfumo Wa Nest.
“Nimefurahishwa na kauli mbiu ya jukwaa hili inayosisitiza “Matumizi ya Kidigitali kwa ajili ya Ununuzi Endelevu katika Sekta ya Umma”. Ninapenda kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ipo mstari wa mbele kuhakikisha kauli mbiu hii inatekelezwa kwa vitendo na ndio maana tumeuzindua mfumo wa ununuzi kwa njia kielektroniki wa NeST ambao utaleta mapinduzi na uwazi katika sekta hii.”amesema Mwingulu.
Hata hivyo jukwaa la PPRA linatarajiwa kufanyika Sudani kusini mwaka 2025 ambapo wamekabidhiwa zawadi kama ishara ya kukabidhiwa kijiti na nchi wenyeji Tanzania
Amesema kuwa,kupitia Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma, Sura Na. 410, taasisi zote za umma zinapaswa kufanya hatua zote za ununuzi kupitia mfumo wa NeST,lengo ni kuhakikisha matakwa ya sheria hiyo yanazingatiwa, pia kuongeza uwazi, uwajibikaji, ushindani na thamani ya fedha zinazotumika katika shughuli hiyo.
Mwigulu ameongeza kuwa anatamani sana kuona nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zinatekeleza kazi za ununuzi na ugavi kupitia mifumo ya kielektroniki, kama huu uliozinduliwa hapa. Jambo hili linawezekana na litafanyika kwa ufanisi zaidi kupitia ziara za mafunzo kutoka nchi moja mwanachama kwenda nyingine, kubadilishana wataalamu na hata kubadilishana uzoefu.
Amewataka kuzitumia fursa hizo kuimarisha shughuli hizi, kwa manufaa ya nchi zetu. Na wa kufanya hivyo, tutaweza kuchangia katika jitihada za viongozi wa nchi zetu katika Jumuiya ya Afrika ya Mashiriki za kuinua hali ya kiuchumi ya wananchi waliomo katika jumuiya hii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma PPRA Dkt. Leonada Magika amesema Tanzania itaendelea kurekebisha makosa madogo madogo yatakayojitokeza kwenye mfumo wa manunuzi wa kidijitali uliozinduliwa ili ulete ufanisi.
Katika mkutano huo wa siku tatu wa mamlaka za udhibiti wa manunuzi wa umma kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki umekutanisha wajumbe zaidi ya 1500.