Rai hiyo imetolewa na kamishina wa SMAUJATA taifa Muhandisi Hashim Omary Ramadhani wakati akizungumza na wachezaji wa timu za kata ya Kirumba na Kiseke katika uwanja wa shule ya msingi Sabasaba ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya The Angeline Jimbo Cup 2024 ambapo amewaasa kucheza kwa kutanguliza upendo, amani na mshikamano ili kuleta jamii iliyo sawa
‘.. Hata katika michezo kuna vitendo vya kikatili vinaweza kufanyika, Kumchezea mwenzako rafu ukamvunja miguu kwa makusudi huo ni ukatili kwasababu watoto wake au ndugu zake watakosa huduma sababu yako ..’ Alisema
Aidha Kamishina Hashim amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kuasisi mashindano hayo huku akiwataka Vijana kuyatumia kwa manufaa ili kuonyesha vipaji vyao
Doto Wilson Tangija ni nahodha wa timu ya kata ya Kiseke ambapo amefafanua kuwa timu yake imeweza kuibuka mshindo katika mchezo huo kwa kuwa wameweza kuzingatia maelekezo ya mwalimu na kuyafanyia kazi makosa yaliyofanywa na wapinzani wao wakati wa mchezo
Akitamatisha mchezaji wa timu ya kata ya Kirumba Evasto Sijali mbali na kumshukuru Mbunge wa Jimbo hilo kwa mashindano hayo ameahidi kujiandaa vizuri kwaajili ya msimu ujao ili makosa walioyafanya yasiweze kujirudia tena na kupata ubingwa
Mechi ya Timu ya kata ya Kirumba dhidi ya timu ya kata ya Kiseke imetamatika kwa timu ya Kiseke kuibuka na ushindi wa goli moja kwa sifuri hivyo kufuzu hatua ya robo fainali