Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo ametoa maelekezo matano kwa Jeshi la Polisi ambapo amewasihi kuimarisha nidhamu, kwa Jeshi la Polisi, kuimarisha usalama wakati wa chaguzi zijazo, kuendelea kudhibiti ajali za barabarani, kuboresha mazingira ya Polisi ngazi ya kata/shehiya pamoja na kuendelea kutekeleza mapendekezo ya Haki Jinai nchini
Sillo amezungumza hayo kwenye halfa ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi sambamba na kusheherekea miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi, mkoani Kilimanjaro Septemba 12, 2024
Mhe. Sillo alilitaka Jeshi la Polisi kuendelea kuimarisha maadili na nidhamu kwa kuwa Jeshi lisilokuwa na nidhamu haliwezi kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa watendaji wake
“Nisisitize kuendelea kuimarisha maadili ndani ya ya Jeshi la Polisi kwani nidhamu ndio msingi wa mafaniko katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku” Amesema Sillo
Pia alitumia fursa hiyo kuwapongeza Askari wote waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyo na imani kubwa na Jeshi la Polisi
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ally Gugu alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kuimarisha usalama wa raia pamoja na mali zao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na wananchi alitoa msisitizo kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaendelea kuratibu na kuwezesha majukumu ya Polisi kwa lengo la kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo
IGP, Camilius Wambura alihitimisha kwa kusema Jeshi la Polisi limejiimarisha zaidi katika mkakati wa kuzuia uhalifu alitoa rai kwa jamii kuhakikisha wanalea familia katika misingi na desturi nzuri za kitanzania ili kuepuka Mmomonyoko wa maadili ambao ndio chanzo cha uhalifu nchini