Na Sophia Kingimali.
Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB). Imetoa rai kwa wanufaika wa mikopo hiyo ambao tayari wanavipato waweze kurejesha mikopo hiyo kwani sasa wameshirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanawafikia wanufaika wote nchini.
Rai hiyo imetolewa leo Septemba 11,2024 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji HESLB, Bill Kiwia wakati ya Hafla ya kubadilishana hati za makubaliano na wadau wa kimkakati ambao ni NIDA,RITA NA ,taasisi ya uchakataji wa taarifa za waombaji mikopo kwenye taasisi za fedha CREDIT INFO
Amesema kuwa lengo la kubadilishana hati za makubaliano na taasisi hizo ni kuweza kuongeza mbinu ya kuwapata wadaiwa sugu wa mikopo hiyo hususani wale walioko kwenye sekta binafsi na isiyo rasmi kwa matumizi ya mifumo ya tehama.
“Bodi ya mikopo inatoa rai kwa wanufaika wa mikopo Hiyo ambayo walipewa ili waweze kurejesha mikopo kwa wakati ili wengine waweze kwenda vyuoni kuendelea na masomo huku Taasisi Ya Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, wakala wa usajili ,ufilisi na udhamini RITA,taasisi za uchakataji wa taarifa za waombaji mikopo kwenye taasisi za fedha CREDIT INFO zikiwa tayari kwa majukumu ya kuwasaka wadaiwa hao”,amesema.
Aidha MKurugenzi Kiwia ameongeza kuwa katika ukusanyaji wa mikopo hiyo wamekaribisha wadau hao katika kwenda kufikisha ujumbe huo kwa wafaidika kwa kutumia Mifumo ya tehama.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi mkuu kutoka
Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA Deusdedit Buberwa amesema kuwa wanashirikiana vyema katika kutekeleza makubaliano ya serikali huku taasisi za kiserikali zikiweza kuunganisha mifumo ya tehama katika kutoa huduma kwa wananchi.
Naye, Mtendaji mkuu kutoka Wakala wa usajili na Ufilisi RITA. Frank kanyusi amesema kuwa watashirikiana na Bodi ya mikopo kuhakikisha wanamrahisishia muombaji taratibu za usahili katika kuomba mikopo hiyo.
Amesema mafanikio hayo yamefikiwa kufuatia kufuata agizo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutaka taasisi za serikali mifumo yao inasomana mpaka ifikapo Disemba.
“Tumeunganisha mfumo wetu na Bodi ya mikopo hivyo muombaji hana haja ya kusumbuka sasa anapoingia kwenye mfumo anaweza kufanya kila kitu hivyo nitoe rai kwa waombaji kuutumia vyema mfumo huo”,amesema.
Pia,Mtendaji huyo amewataka wanafaika wa mkopo kuhakikisha wanalipa mkopo wao ili mikopo hiyo iweze kuwasaidia wengine.
Naye,Mtendaji mkuu wa taasisi za uchakataji wa taarifa za waombaji mikopo kwenye taasisi za fedha CREDIT INFO CREDIT INFO Edwin Urasa amesema kuwa wanufaika wa mikopo hiyo ya elimu ya juu ambao wanakipato tayari wanapaswa kulipa mikopo yao kwa uaminifu kabla ya kuanza kufuatiliwa.
“Niwasihi wanufaika waanze kujitokeza na kurejesha mikopo kwa wakati sahihi ili taasisi za fedha ziweze kukopesha wanavyuo wengine ambao wanatarajia kwenda vyuoni”,amesema. as