Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Arusha leo kuhusu uzinduzi huo.
………
Happy Lazaro, Arusha .
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kesho Septemba 11, 2024 anatarajiwa kuzindua taarifa ya tathimini huru na ya kina ya miaka mitano ya utekelezaji wa mpango wa kuboresha Mazingira ya Biashara nchini Tanzania.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo akizungumza kwenye Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kanda ya Kaskazini amesema kuwa zoezi la uzinduzi huo litafanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es salaam kuanzia majira ya saa kumi na moja jioni.
Prof. Kitila amesema mpango huu ulikuwa na lengo la kufanya uchambuzi wa mazingira ya biashara nchini na kuanisha mageuzi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kutatua changamoto na kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini Tanzania.
“Mkumbi uliainisha maeneo makubwa matatu ya kushughulikia katika kuboresha mazingira ya biashara nchini,ambapo maeneo haya ni gharama za kufanya biashara,mlolongo mgumu na mrefu wa kupata vibali vya kufanya biashara ,na uwepo wa utitiri wa mamlaka za udhibiti zinazorekebu shughuli za biashara nchini”.
Aidha amesema kuwa, serikali iliajiri mtaalamu mshauri kufanya tathmini huru a ya kina ya miaka mitano ya utekelezaji wa MKUMBI kufuatia kukamilika kwa taarifa ya tathmini hiyo .
Prof.Mkumbo ameongeza kuwa,pamoja na mambo mengine ,tathmini imeonesha mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa MKUMBI na changamoto mpya zilizojitokeza na mapendekezo ya hatua zaidi za kuchukua katika kuendelea kuimarisha na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Aidha Waziri Mkuu pia atazindua Taarifa ya Hali ya uwekezaji nchini kwa mwaka 2023, Mwongozo wa uanzishaji na uendeshaji wa Kanda Maalum za Kiuchumi (Special Economic Zones)pamoja na kuzindua mpango Mkakati wa Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji.