Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania ‘Taifa Stars’ imefufua matumaini ya kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2025) baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Guinea katika mchezo wa pili wa kundi H uliopigwa katika uwanja wa Charles Kanan Benny de Yamoussoykro.
Katika mchezo huo Taifa Stars ililazimika kutokea nyuma baada ya mshambuliaji wa Lille ya Ufaransa Mohamed Lamine Bayo kuanza kuwafungia Guinea dakika ya 57.
Lakini nyota wa Azam Fc Feisal Salum Abdallah akaisawazishia Tanzania dakika 61 kabla ya kiungo mwenzake Mudathir Yahya Abbas kufunga bao la ushindi dakika ya 88.
Kufatia matokeo hayo yanaibakisha Taifa Stars nafasi ya pili ikiwa na pointi nne, nyuma ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi tisa, huku Guinea inaendelea kushika mkia nyuma ya Ethiopia yenye pointi moja.