Mkoa wa Mara umevuka malengo katika zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ambapo idadi ya watu wapya waliojitokeza kujiandikisha ni kubwa ikilinganishwa na idadi iliyokuwa imekadiriwa kuandikishwa Mkoani humo.
Akizungumzia zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanal Evans Mtambi amewapongeza wananchi nakuwataka kutumia wingi waliojitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kufanya hivyo pia katika Uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu.
Kwa upande wake Dominicus Rusasi ambaye alikuwa mratibu wa zoezi hilo la uandikishaji amesema maeneo ya Mipakan wamehakikisha Mkoa wa mara umeandikisha watu sahihi naeneo yaliyokuwa na watu wengi pia waliongeza vitendea kazi kutokana na Tume ya uchaguzi ilikuwa imejipanga vyema na zoezi hilo.