Na: Mwandishi Wetu, Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ummy Ally Mwalimu leo Septemba 8, 2024 ameshiriki zoezi la ufunguzi wa mafunzo ya Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) wa wilaya ya Tanga.
Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ambapo Ummy Mwalimu aliwasihi vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwakani.
Aidha, Ummy Mwalimu amesema CCM ni chama cha wanachama wote wala hakuna mmiliki wa chama, hivyo mwanachama yeyote anayo haki ya kugombea nafasi huku alisisitiza kuwa nafasi ya Urais pekee ni ya Dk. Samia Suluhu Hassan lakini nafasi nyingine zote zipo wazi kwa mwanachama yeyote mwenye sifa anayo nafasi ya kugombea.
Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Ummy Mwalimu amewahakikishia kuwa yupo pamoja na UVCCM wa wilaya ya Tanga katika kuhakiksha chama kinaibuka na ushindi wa kishindo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka huu.
Katika hatua nyingine, kutokana na umuhimu wa kusajili wanachama wapya, Ummy Mwalimu ameahidi kutoa Simu Janja (Smart phone) nane (08) ili kuongeza wigo wa usajili wa wanachama wapya wa CCM. Vilevile, Ummy Mwalimu ameahidi kutoa kutoa sare 500 za vijana wa hamasa pamoja na sare 50 za vijana wa Itifaki.