Mkurugenzi  mkazi wa CBM International na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya Azaki,Nesia  Mahenge akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha
….
Happy  Lazaro,Arusha .

Waziri wa mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo anatarajiwa kuwa mgenirasmi katika ufunguzi wa wiki ya azaki inayotarajiwa kuanza  kesho Septemba 9 hadi 13 mwaka huu mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha ,Mkurugenzi  mkazi wa CBM International na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya Azaki,Nesia  Mahenge amesema kuwa zaidi ya watu 600 wanatarajiwa kushiriki katika wiki hiyo pamoja  na mashirika zaidi ya 400 kutoka ndani na nje ya nchi ambapo wanakutana kuongeza nguvu  ya pamoja na kuweza kuzungumzia swala la maadili ya nchi yetu kuhakikisha wanayalinda na kuyatunza. 
Amesema kuwa ,wamekuwa wakiadhimisha  wiki hiyo kila mwaka na wamekuwa wakija na timu tofauti na kuweza kufanya tathmini kwa kujifunza vitu vya kuweza kuboresha na kujifunza kutoka kwa jamii mbalimbali .
“Zaidi ya  vijana 70 wanatarajiwa kushiriki katika wiki hiyo ambapo watapata fursa ya kuweza kujifunza maswala mbalimbali juu ya ushiriki wao katika demokrasia  na namna wanavyotakiwa  kushiriki katika shughuli za  ujenzi wa Taifa “amesema Mahenge .
Ameongeza kuwa ,kupitia maadhimisho  hayo ambayo kufanyika kila mwaka yameleta mafanikio makubwa sana kutokana na wananchi kuweza kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwa wengine. 
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha sekta za umma kutoka benki ya Stanbic  , Doreen Dominic  amesema kuwa,wamekuwa wakifanya wiki hiyo kwa mfululizo  mwaka wa  sita  sasa huku lengo kubwa likiwa ni kupaza sauti ya pamoja katika maswala mbalimbali .
Ameongeza kuwa,kupitia wiki hiyo  wanaungana na taasisi mbalimbali katika  kufanya maboresho mbalimbali na kujadili sauti ya pamoja na kuhakikisha wanapigania haki za watanzania wote waliopo katika maeneo mbalimbali ili waweze kupata haki.zao za msingi .
Mkurugenzi wa Haki elimu ,John Kalaghe   amesema kuwa kupitia wiki hiyo kutakuwepo na kipindi   cha vijana ambapo wataweza kushiriki kikamilifu na kujadili juu ya ushiriki wao katika kuandaa majadiliano kwa vijana  juu ya nafasi zao na ushiriki wao katika.nafasi mbalimbali. 
“Kuna umuhimu   mkubwa kwa vijana kushiriki katika michakato ya kidemokrasia kwani bado  ushiriki wao ni hafifu ,na wanataka kuona vijana  na wanawake wanashiriki kikamilifu katika kuchagua  viongozi wenye  uadilifu na weledi wa hali ya juu. “amesema .
Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania Tanzania (TGNP),Lilian Liundi amesema kuwa,zaidi  ya waandaaji 20 kutoka asasi za kiraia wakishirikiana katika kuandaa wiki  hiyo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni sauti,dira na dhamani. 
Liundi amesema kuwa,mwaka huu wanataka sauti ya mwananchi iweze kusikika kwani kuna umuhimu wa kuweka sauti za wadau wote na upana wao kuhusu kuzungumza maswala mbalimbali. 
“Tunataka kuona sauti za watu mbalimbali  zinasikilizwa huku wanawake tukitaka  watoe sauti zao na kusikilizwa na kuangalia dira  ya 2050 kuhusu maswala ya wanawake na uwekezaji katika dira kwani tunataka swala la uwekezaji liwe  kipaumbele.”amesema .