Mkurugenzi wa Kampuni maarufu ya utalii inayofahamika kama M Tours, Bi. Elvera Verhagen akiwa ameambatana na babu yake Bw. Van Denzel kutoka Uholanzi tarehe 6/9/ 2024, walitembelea eneo la Makuyuni Wildlife Park liliopo wilayani Monduli jijini Arusha kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo na kupata fursa ya kufahamu namna wanavyoweza kufanya biashara ya utalii katika eneo hili hasa Utalii wa Kuendesha Baiskeli.
Uwepo wa miundombinu wezeshi ya barabara, wingi wa wanyamapori na mandhari ya kuvutia huifanya Makuyuni Wildlife Park kuwa chaguo bora kwa mtalii yeyote wa ndani na nje ya Tanzania.
Shughuli nyingine za kitalii zinazoweza kufanyika katika eneo hilo ambalo ni makazi ya wanyamapori wakubwa wanne (Big Four) ambao ni Nyati, Simba, Tembo, ni pamoja na kupanda mlima (Hiking), utalii wa kutembea kwa miguu (Walking Safari),Utalii wa kuona ndege, jua likichomoza na kuzama, utalii wa Utamaduni (jamii ya kabila la wamasai inayozunguka eneo hili).
Makuyuni Wildlife Park ni eneo lililo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA ambalo Mamlaka hiyo ilikabidhiwa na Serikali hivi karibuni ili iweze kulisimamia na kuliendeleza ikiwa na pamoja na kulinda rasilimali wanyamapori zilizopo katika eneo husika.