Na Sophia Kingimali.
Mama wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini hayati Steven Kanumba, Frola Mtegoa amepongeza waandaji wa Tamasha la kuwakumbuka wasanii mbalimbali wa filamu,Muziki na waandishi wa Habari lililojulikana kama FARAJA YA TASNIA kwani kitendo hiko kimeweza kuwagusa na kuwakumbusha mazuri na mema waliyoyafanya katika tasnia na Taifa kwa ujumla.
Hayo ameyasema leo Septemba 7,2024 jijini Dar es salaam katika viwanja vya Leaders ambapo tamasha hilo linaendelea amesema tamasha la Faraja ya Tasnia ambalo linalenga kuwaenzi wasanii na wanatasnia wote waliotangulia Mbele za haki limekuwa na tija na faraja kwa ndugu pia walioondokewa na ndugu zao.
Aidha Mama Kanumba ameongeza kuwa kuwa walioofikiria kuja na tamasha hilo wamefanya jambo jema kwani kuwaenzi wasanii na wengine walio kwenye tasnia ni moja ya njia ya kuonesha kuwa watu hao bado wanathamini wa jamii.
Aidha Mama kanumba Amesema kuwa Leo ni siku ya faraja kwani Bado anamkumbuka mwanae mpaka Leo
”Leo ni siku muhimu kwangu kabla ya kuja hapa nilivyoamka nililia sana namkumbuka mwanangu lakini niombe tamasha kama hili liendelee kwani inasaidia hawa watu kubaki kwenye mioyo ya wapendwa wao”.Amesema mama kanumba
Kwa upande wake Msanii wa Maigizo nchini Vaileth malle(Mama Afrika) amesema kumbukumbu hii imekuwa ya historia kwao kwani wameweza kuwakumbuka wanatasnia lakini pia wataendelea kuyaenzi yale yote mazuri waliyoyafanya.
Tamasha la Faraja ya Tasnia limeandaliwa na msanii Steve Nyerere na linafanyika katika uwanja wa Leaders Club,Kinondoni ambapo limeudhuliwa na viongozi na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki
Miongoni mwa wanatasnia wanaoenziwa kwenye tamasha hilo Ni pamoja na Marehemu Steven Kanumba,Albert MaNgwair,Amina Chifupa,Mzee Matata,James Dandu(mtoto wa Dandu),Ruge Mutahaba,Mzee Majuto,Sajuki,Godzilla,Sharrron Milionea,Kibonde,Mandojo,Gardner G Habash,Remi Ongala,Maunda Zorro,Captain Komba,Bi Kidude,na wengine