RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiangalia ngoma za Utamaduni wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji,baada ya kumalizika kwa uwekaji wa Shada la Maua katika Mnara wa Mashujaa Viwanja vya Matora, wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Msumbiji yaliyofanyika leo 7-9-2024, na (kushoto kwa Rais) mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa Mshumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akiwa na Mkewe Mama Isaura Nyusi, wakisalimiana na Wananchi baada ya kumalizika kwa hafla ya uwekaji wa Shada la Maua katika Mnara wa Mashujaa katika viwanja vya Matora Msumbiji leo 7-9-2024, wakati wa Sherehe za Maadhinisho ya Ushindi wa Msumbijin.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, mgeni rasmin katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Msumbiji, akipata maelezo ya picha mbalimbali za historia ya ukombozi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, wakati akitembelea maonesho hayo katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji, na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, mgeni rasmin katika Sherehe za Maadhimisho ya Miako 50 ya Ushindi wa Msumbiji, akimsikiliza mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akielezea picha mbalimbali wakati akitembelea maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji leo 7-9-2024.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum kutoka kwa Wananchi wa Matora, wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Matora leo 7-9-2024, na (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji wakimsikiliza mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji leo 7-9-2024.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji leo 7-9-2024.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Askari walioshiriki katika mapambano ya kuikomboa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, wakishiriki katika gwaride maalumu la Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji wakipita katika jukwaa kuu la Viongozi katika uwanja wa mpira matora Msumbiji, wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika leo 7-9-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji, maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya mpira Matora Msumbiji leo 7-9-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akizungumza na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akiwa na Mkewe Mama Isaura Nyusi, wakiondoka katika uwanja wa mpira wa Matora baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Ushindi wa Jamhuri ya Watu wa Msumbiji iliyofanyika katika uwanja huo leo 7-9-2024.(Picha na Ikulu)