Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
7, Sept,2024
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa CCM, Ally Salum Hapi, akiwa Kibaha Vijijini, amesisitiza umuhimu wa viongozi walioko madarakani kuwajibika kwa wananchi waliowapa nafasi ya uongozi.
Hapi ameonya kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, chama kitaunga mkono wagombea wanaokubalika na wananchi, ili kuondoa mzigo kwa Chama.
Hapi alieleza, chama kinahitaji wagombea watakaochaguliwa na wananchi wenyewe, na sio wale watakaotafuta kura kwa njia zisizo za kiungwana.
Aliwaonya viongozi dhidi ya kulalamika baada ya kushindwa, akiwakumbusha kuwa uwajibikaji kwa wananchi ndio njia ya uhakika ya kupata ridhaa yao.
Vilevile, Hapi alisisitiza umuhimu wa viongozi na wanachama wa CCM kukutana katika vikao rasmi vya chama ili kutatua changamoto zinazowakabili kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na chama.
Nae, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao, aliwalaumu wale wanaosababisha mivutano ndani ya chama, hali inayoweza kudhoofisha uhusiano na wananchi.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Kibaha Vijijini,Kanusu alibainisha kuwa migogoro ndani ya chama sio kubwa, bali inasababishwa na jeuri ya baadhi ya wanachama.