……..,………….
Save the Children Tanzania imesikitishwa na kifo cha mtoto wa miezi sita huko Dodoma baada ya kudaiwa kufanyiwa
unyanyasaji wa kijinsia na mtu anayetambulika kuwa ni baba yake,usiku wa tarehe
1 Septemba 2024.
Kwa mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na Shirika Hilo imesema Tukio hilo la kusikitisha lilitokea katika Kata ya Kizota,na polisi kwa wanaendelea na uchunguzi ili kubaini mazingira ya kifo cha mtoto huyo.
Polisi wamemkamata mshukiwa kama sehemu ya uchunguzi wanaoendelea kufichua ukweli wa tukio hilo la kuhuzunisha.
Taarifa hiyo imesema kuwa Kifo cha
mtoto mchanga kama huyo ni
ukumbusho wawazi juu ya mambo yanayowakumba watoto lakini pia
inawakumbusha umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti za ulinzi wa watoto nchini Tanzania.
“Tukio hilo la kusikitisha niukumbusho thabitiwa jinsi ilivyomuhimu kwakilamtu
kuchukua hatua kulinda watoto wetu.Nihuzuni kuona wale ambao wanawaamini
na wanapaswa kuwalinda kwa ukaribu,kama baba,wanazidi kuwa
wanyanyasaji/wanatenda ukatili.Tunatoa wito kwa mamlaka husika kuharakisha na
kufanya uchunguzi wa kina wakesi hii na kuchukua hatua stahiki za kuzuia matukio kama haya siku zijazo.Lakini pia tunahitaji kushirikia na kama jamii ilikuunda mazingira salama ambapo watoto wanaweza kukua bila hofu na madhara .Save the Children imejitolea kufanyakazi na jamii za mitaa,serikali,nawashirika wetu ili
kuboresha ulinzi wa watoto na kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kustawi, kupata elimu bora,nakuwasalama.”alisema Mkurugenzi Mkazi wa Save the Children,Angela Kauleni,