………………..
Na Sixmund Begashe – Morogoro
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili Benedict Wakulyamba amewasili Hifadhi ya Taifa Mikumi, na Kikosi kazi chake ambao ni Maafisa waandamizi kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo kukutana na Manejime ya Hifadhi hiyo, kutoa mafunzo kwa askari wa Jeshi la Uhifadhi na kukagua shughuli za maendeleo Hifadhini humo.
Akiwa kwenye darasa maalum la Maafisa na Askari wa Hifadhi hiyo, CP. Wakulyamba amesisitiza ufanyaji wa kazi uzingatie falsa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo ni
Maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resilience) Mabadiliko (Reforms) Kujenga Upya (Reconstruction) katika Kuimarisha Maridhiano kwa mahusiano mema kazini, Kujenga upya fikra katika Utendaji kazi wa kila siku, Kubadilika na kuacha kufanya kazi kwaemazoea, na kuwa na ustahimilivu.
Aidha CP. Wakulyamba amewataka askari hao kuzingatia mafunzo waliyopewa na Maafisa wa Polisi Mrakibu wa Polisi Joseph Jingu na Mrakibu wa Polisi Ocsar Felician juu ya Haki Jinai yanayotekelezwa kutokana na agizo la Tume ya Haki Jinai ili Kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi hilo.
Akikagua ujenzi wa Kituo cha Taarifa kwa wageni kinachotekelezwa na Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), CP. Wakulyamba amemtaka Mkandarasi kuongeza Kasi ili ujenzi wa Kituo hicho ukamilike kwa haraka kwa kuwa ni muhimu kwa maendeleo ya Hifadhi ya Mikumi na Taifa kwa ujumla.