*Ni matokeo ya ziara ya Rais Samia nchini humo
Dar es Salaam
Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Madini, Taasisi zake pamoja na Wataalam kutoka Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma wanaotarajia kushiriki mafunzo ya muda mfupi katika Taasisi ya Jiolojia ya nchini India waliagwa rasmi Septemba 2, 2024 katika Ofisi za Ubalozi wa India nchini.
Wataalam hao wanatarajiwa kupata mafunzo ya kujengewa uwezo katika masuala yanayohusu shughuli za utafutaji madini.
Ushiriki wa wataalam katika mafunzo hayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya Tanzania na India ambapo yalichagizwa zaidi kufuatia ziara aliyoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Hassan nchini humo.