Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini Mhandisi Victor Seif akizungumza katika Kikao kazi kati ya Jukwaa la Wahariri na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kilichofanyika leo Septemba 02, 2024 kwenye ukumbi wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Sabato Kosuri akizungumza katika Kikaukazi hicho kabla ya kuanza kuwa uwasilishaji wa mada kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seif.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA Bi. Catherine Sungura akishiriki katika Kikaukazi hicho.
………………
WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), umesema mtandao wa barabara za wilaya umeongezeka kutoka kilomita 108,946 .19 hadi kilomita 144,429.77 kufikia Juni 2024.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini Mhandisi Victor Seif akizungumza katika Kikao kazi kati ya Jukwaa la Wahariri na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kilichofanyika leo Septemba 02, 2024 kwenye ukumbi wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es Salaam.
“Kwa upande wa changarawe hadi kufikia Juni mwaka huu barabara za wilaya zimefikia kilomita 42,059.17 na lami kilomita 3,0337.66.
“Wilaya ya Rufiji zimejengwa kilomita 32 kwa kutumia teknolojia ya kokoto (Ecozyme) na Wilaya ya Itilima kilomita 5.2, tunatumia malighafi kama mawe ambayo hupunguza asilimia zaidi ya 50 ya gharama na tayari tumejenga madaraja 275 na kilomita 225 za barabara kwa kutumia mawe,”alisema Seif.
Seif, alisema hadi sasa kwa kutumia teknolojia hiyo jiji la Dodoma tayari kilomita moja imejengwa na Wilaya ya Chamwino kilomita 6.95 na zote zimekamilika.
“Tathimini iliyofanyika mwaka 2022/2023 ilibaini Sh. Trilioni 1.35 zinahitajika kuanzia 2023/2024; ili asilimia 85 ya mtandao wa barabara za wilaya zipitike misimu yote, sasa Tarura inapata wastani wa Sh. Bil. 850 kwa mwaka,”alisema. Seif.
Aidha, Seif alisema kipaumbele kingine ni kupandisha hadhi barabara za udongo kuwa za changarawe kuwa lami, kwa kuzingatia vipaumbele vya kiuchumi kitaifa na kimataifa.
Akizungumzia ujenzi Mkoa wa Dar es Salaam, Seif, alisema, nyumba nyingi katika mkondo wa maji.
Alisema kutokana mazingira hayo, Mradi wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam awamu ya Pili (DMDPi II), unakwenda kuboresha maeneo mengi ya jiji hilo.
“Mradi huu utakuwa ndani ya Halmashauri tano za jiji la Dar es Salaam na utatekelezwa kwa miaka sita, barabara kilomita 250 zitajengwa, mifereji ya kilomita 90; vituo vya mabasi tisa, masoko 18; madampo matatu na wanufaika wa mradi ni wananchi wa milioni 3.98,”alisema Seif.