RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye maadhimisho yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumapili Septemba 1, 2024.
(PICHA NA JOHN BUKUKU -DAR ES SALAAM)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye maadhimisho yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumapili Septemba 1, 2024 akiwa na Mkuu Majeshi ka Ulinzi na Usalama Jenerali John Jacob Mkubwa.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipiga saluti wakati wimbo wa taifa ukioigwa katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye maadhimisho yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumapili Septemba 1, 2024.
Msafari wa magari ya RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan ukiingia katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye maadhimisho yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumapili Septemba 1, 2024.
Mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Amani Karume mama Fatuma Karume akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila wakati alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kuhudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ) kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Msraafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila alipowasili kwenye uwanja wa uhuru katika maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdory Mpango akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax alipowasili kwenye uwanja wa Uhuru katika maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila wakati alipowasili kwenye uwanja ja wa Uhuru kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ kulia nia Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena
Rais Mstaafu wa Zanzibar Abeid Amani Karume aliwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi la Wananchi wanTanzania JWTZ.
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila wakati alipowasili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kushiriki maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ kulia ni Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax.
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Mosses Kusikika akiwasili kwenye uwanja wa uhuru katika maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ.
…………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litaendelea kuimarika katika nyanja zote kwa kufanya mabadiliko ya Teknolojia ikiwemo zana, vifaa, mikakati, mbinu za medani ili kuliwezesha kutimiza uwajibu wake ipasavyo.
Akizungumza leo Septemba 1, 2024 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Samia, amesema kuwa miaka 60 ya JWTZ yamekuwa na mafanikio makubwa kwa kutimiza majukumu yao kikamilifu na ufanisi mkubwa.
Dkt. Samia amesema kuwa jeshi limefanya kazi kubwa ya kulinda Muungano na Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar, uhuru, katiba na mipaka ya nchi ikiwemo ardhini, angani pamoja na maji.
Amesma kuwa JWTZ J limeshiriki na kufanikisha harakati za ukombozi wa bara la Afrika na kuwa mstari wa mbele katika vita vya ukombozi katika nchi mbalimbali ikiwemo Msumbuji, Angola, Zimbambwe, Afrika Kusini na kurejesha heshima na utu katika nchi hizo.
“Jeshi letu limeendelea kushiriki kikamilifu na kuwa na mafanikio makubwa katika operesheni za kulinda amani katika nchi mbalimbali ikiwemo Sudani, Msumbiji, Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na DRC Kongo” amesema Dkt. Samia.
Amesema kuwa jeshi linafanya kazi ya kuwalea watanzania kwa kuwafundisha kazi, maadili na kujitengemea kupitia Jeshi la kujenga Taifa (JKT). “Jeshi litaendelea kuwa la kisasa na madhubuti zaidi lenye zana na nyenzo za kisasa pamoja na kudumisha misingi ya kuanzishwa kwake” amesema Dkt. Samia.
Dkt. Samia amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kutimiza uwajibu wa kikatiba kwa kulinda amani ya nchi na kukemea uvunjifu wa amani katika Nchi.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzani Jenerali Jacob John Mkunda, amesema kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa uweledi na uzalendo wa hali ya juu kwa kuzingatia na kuviishi viapo vyao.
Jenerali Mkunda amesema kuwa katika maadhimisho ya miaka 60 wamekuwa na matukio mbalimbali ikiwemo mazoezi ya pamoja kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la China, mashindano ya Kombe la CDF, zoezi la medani la miaka 60.
Jenerali Mkunda amepongeza jitihada zilizofanywa na maafisa na askari wa JWTZ tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo.