OR – TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kuhakikisha wanafunzi walio katika shule zote za kutwa za umma na binafsi wanapata chakula bila kujali ni wa madarasa ya mitihani ama lah na kamati za shule ziimarishe usimamizi wa chakula kinachotolewa na wazazi kwa ajili ya mpango wa chakula shuleni.
Pia amewataka kuendelea kusimamia kikamilifu fedha zote zinazopangwa za kutekeleza afua za lishe na kusimamia ubora wa taarifa ili taarifa zinazoletwa katika ngazi za juu ziwe zinaakisi uhalisia katika jamii.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa mkutano wa tathimini ya mkataba wa lishe na kutambulisha mpango wa taifa wa uwekezaji katika afya ya mama na matoto nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa Jiji – Dodoma kuanzia tar 30 – 31 Agosti,2024.
Pia amesema kwa Shule za bweni zinazopata fedha kwaajili ya chakula ni vyema kuhakikisha chakula kinachutumika mashuleni ni kile kilichoongezewa virutubishi na ameelekeza wazabuni wa chakula shuleni kupeleka chumvi yenye madini joto,unga na mafuta ambayo hayameongezwa virutubishi.
Pia amewataka kusimamia ubora wa huduma za Afya na kutokomeza kabisa malalamiko ya wananchi dhidi ya ubora wa huduma na vitendo vingine vinavyochonganisa Serikali na wananchi na kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya.
Kwa upande wa Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya kujipanga kutoa elimu kuhusu bima ya afya kwa wote na kuhakikisha wanafanya kampeni ya mtu ni afya ili kuondoa magonjwa ya mlipuko hasa magonjwa ya kipindupindu.
“Kwa uwekezaji ambao umefanywa na serikali katika utoaji wa huduma za afya tukishindwa kukiondoa kipindupindi tutakuwa hatujitendei haki sisi watanzania.”
“Pia twendeni tukapambane tukahakikishe uonjwa wa homa ya nyani hauingii ndani ya nchi yetu, tukishakosea kidogo na ugonjwa ukaingia nchini madhara tutakayopata ni makubwa na kuundoa inaweza kuwa kazi ya ziada.”
Alisema pia Wizara yake itaendelea kufanya ziara maalum za matibabu ya kibingwa kwa kuwatumia madaktari wa ndani ya nchi mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kama.
Aidha, Jenista alisema katika kuhakikisha mikataba ya lishe inatekelezwa kwa tija, Wizara yake itahakikisha inakamilisha kwa haraka Sera ya Taifa ya Chakula na Lishe na kushirikiana na sekta binafasi ili chakula cha watoto mashuleni kiongezewe virutubisho