Na Prisca Libaga Tanga
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 29.08.2024 yatoa elimu juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya katika Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Tanga.
Kauli Mbiu ya Jukwaa hilo ilikuwa ni; “_Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali ni Wadau Muhimu, Washirikishwe Kuimarisha Utawala Bora_”
Jumla ya wadau zaidi ya 120 wa Asasi za Kiraia walishiriki kutoka Wilaya na Halmashauri zote za Mkoa wa Tanga.
Aidha, mgeni rasmi wa Jukwaa hilo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda S. Burian. Pia, mgeni maalum alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Kuratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Mwantumu Mahiza.
Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha mashirika yanayojihusisha na miradi ya makundi ambayo yapo kwenye hatari ya kuingia kwenye tatizo la dawa za kulevya hususani vijana na wanafunzi, basi mashiriki hayo yaanze kufanya na shughuli za uelimishaji juu ya tatizo hilo ili kupata Tanga huru isiyojihusisha na matumizi wala biashara haramu ya dawa za kulevya