Picha zikionesha Kiwanda cha uchakataji chumvi ghafi ambacho kinajengwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutatua changamoto ya upatikanaji wa soko wa chumvi ghafi inayozalishwa nchini.
Maandalizi ya ujenzi wa Kiwanda cha chumvi cha mfano kwa ajili Wachimbaji wadogo yanaendelea ambapo hadi sasa mtambo wa kuchakata chumvi unaendelea kutengenezwa nchini India.
Kiwanda hichi cha kuchakata chumvi ghafi kitajengwa katika Wilaya ya Kilwa,Mkoani Lindi.
Ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2024.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake katika mikoa ya kusini mwaka 2023 aliielekeza STAMICO kupitia Wizara ya Madini kuhakikisha inasaidia upatikanaji wa soko la chumvi ghafi inayozalishwa na wazalishaji wa ndani.