Na WAF, Mwanza
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Hamad Nyembea amezitaka Hospitali za Rufaa za mikoa zilizoanza kutoa huduma za Tiba Jumuishi ziwe na Mfumo wa utoaji Tiba ili kusaidia jamii kuondokana na imani tofauti juu ya dawa za Tiba Asili.
Dkt. Nyembea ameyasema hayo Agosti 30,2024 wakati ziara wa Timu ya Tiba Asili kutoka Hospitali za Rufaa nchini walio kutana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure kwenye kikao kazi chenye lengo la kujadili utoaji wa huduma za Tiba Jumuishi
“Upo umuhimu wa kutengeneza Mfumo wa utoaji huduma katika Hospitali zetu za Rufaa ili mgonjwa akifika kupata huduma ya Tiba Jumuishi aweze kupata matibabu kwa wakati” amesema Dkt. Nyembea
Dkt. Nyembera amesema, huduma hizo ili ziwe bora Hospitali zote zinazotoa huduma ya Tiba Asili zinatakiwa ziweze kutenga vyumba maalumu vya huduma ya Tiba Jumuishi kwa Hospitali zetu ili watu wa utafiti waweze kuvitumia kujua ni magonjwa gani yana isumbua jamii.
Dkt. Nyembea ametumia fursa hiyo kuwataka wataalamu wa Tiba Asili kuendelee kutoa elimu juu ya huduma ya Tiba Asili kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa ambazo zimeanza kutoa huduma hiyo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Emmanuel Peter ambao pia ni wazalishaji na wasambazaji wa Dawa za Tiba Asili amesema Taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha na unapima wa ubora wa dawa kabla ya kupelekwa kwa watumiaji.
“Lengo letu ni Kupima ubora wa dawa kabla ya kupelekwa Kwa watumiaji ili tujiridhishe kama dawa zina ubora unaofaa na kwa binadamu.” amesema Dkt. Emmanuel Peter.
Sambamba na hayo Timu hiyo ya Tiba Jumuishi wametembelea na kuupongeza uongozi wa Hospitali ya Sekoutoure kwa kazi nzuri ya kuboresha huduma, usafi wa mazingira na miundombinu bora