Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao iliyofanyika leo Agosti 29, 2024 katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Leah Mnzava akizungumza jambo wakati wa akifungua warsha ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao iliyofanyika leo Agosti 29, 2024 katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Afisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni Neema Mwalubilo akizungumza jambo kuhusu umuhimu wa warsha hiyo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Maafisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni wakiwa katika warsha ya kujengewa uwezo ikiwemo umuhimu wa kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao iliyofanyika leo Agosti 29, 2024 katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Leah Mnzava, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee, Maafisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa warsha ya kujengewa uwezo ikiwemo umuhimu wa kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao iliyofanyika leo Agosti 29, 2024 katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni imewajengea uwezo Maafisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao jambo ambalo litasaidia kuongeza ufanisi na kuleta tija.
Akizungumza leo Agosti 29, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo Maafisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni, Mwanasheria Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Leah Mnzava, amesema kuwa wanatarajia baada ya warsha hiyo maafisa wa ustawi wa jamii watakwenda kutimiza uwajibu wao kwa ufanisi katika maeneo yao ya kazi.
Mwanasheria Mnzava amesisitiza umuhimu wa kutimiza uwajibu wao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi ili kuleta tija katika utendaji kazi na kufikia malengo.
Ameipongeza TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni kwa kutoa mafunzo kwa maafisa wa ustawi wa jamii, huku akitoa wito mafunzo hayo kuwa endelevu ili kuwafikia wadau wengi.
“Tunaomba hii elimu iwafikie wenyeviti, watendaji wa serikali za mtaa na wajume kwa sababu migogoro mingi inaanzia huko na wanakaa karibu na watu wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia” amesema Mwanasheria Mnzava.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Christian Nyakizee, amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa jamii kwani Taifa kinaitaji wananchi wazalendo ambaoh wanakemea vitendo vya rushwa.
Nyakizee amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu kutoka Halmashauri wa Manispaa ya Kinondoni zinaonesha katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24 wamepokea mashauri ya kingono 41 kati ya hayo 37 yaliwahusu watoto.
Amesema kwa mujibu wa takwimu hiyo inaonesha kundi kubwa linaloathiri na ukatili wa kingono ni watoto, hivyo mafunzo haya yatawasaidia maafisa wa ustawi wa jamii kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Amesema kuwa katika kuhakikisha malengo yanafikiwa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni inaendeleea kuwajibika na kufatilia kwa kuongea na wadau ili waweze kutekeleza majukumu kwa uweledi.
“Maafisa wa Ustawi wa Jamii wanapaswa kuzingatia Sheria na kujiepusha na vitendo vya rushwa ikiwemo kufata taratibu na kanuni, kujiepusha na matumizi mabaya ya madaraka” amesema Nyakizee.
Nyakizee ametoa wito kwa Maafisa wa Ustawi wa Jamii kufanya kazi yao kwa kuzingatia maadili.
Nao washiriki wa warsha hiyo akiwaem Afisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni Neema Mwalubilo, amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.