Wazazi na walezi Wilayani Serengeti Mkoani Mara wameaswa kuacha kuingiza tamaa za mali za kuwazuia watoto wakike ili wasijiunge na vyuoo vya ufundi kwaajili ya kuolewa kwani kufanya hivyo nikukatili safari ya maisha yao katika elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa world Changer Vision Tanzania Bw Sulus Samweli katika mahafali ya Saba ya chuo hicho ambapo amesema bado uwepo wa Mila zilizopitwa na Wakati hususan Wilayani Serengeti zinaendelea kuitesa kwa kiasi kikubwa jamii hiyo ambapo Serikali imeombwa kuchukua hatua Kali.
Akizungumza katika Tawala Wilaya ya Serengeti katika mahafali hayo amesema ushirikiano baina ya Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaibua watoto wakike walioachishwa masomo nakuwaresha shuleni.
Baadhi ya mabinti wameiomba Serikali kutunga Sheria Kali ambazo zitasaidia kukomesha vitendo vya namna hiyo