Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amewakaribisha Maafisa kutoka TASFAM mradi wa uwendelezaji na usimamizi wa uvuvi na ukuzaji wa Viumbe Maji Tanzania na Maafisa kutoka Bank ya Dunia (WB) na kuwahakikishia ushirikiano katika utekelezaji wa mradi wao.
Akiutambulisha mradi huo Ndugu Nichrous G. Mlalila ambaye ni Mratibu wa Mradi wa TASFAM amesema kuwa, mradi huo katika ukanda wa kusini unatarajiwa kujenga Mhalo katika maeneo ya ukanda wa kusini ikiwa ni Bagamoyo, Mkuranga, Lindi na Mtwara ambapo Lindi patajengwa na Soko la Uvuvi.
Ndugu Nichrous amesema katika kufanikisha hilo, ameambatana na maafisa kutoka Bank ya Dunia ambao ni wafadhili wa mradi kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mradi huo katika maeneo husika ambayo yamependekezwa . Moja ya sharti la utekelezaji wa mradi huo kutokuwepo kwa migogoro ya ardhi katika eneo ambalo mradi unakwenda kutekelezwa.
kwa upande wake Katibu Tawala amewahakikishia maafisa hao kupata ushirikiano kutoka serikalini ili lengo la mradi lifanikiwe na kuleta tija kwa jamii.
Mradi wa TASFAM unafadhiliwa na Banki ya Dunia (WB) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.