Bw. Laurence Msofe Mkurugenzi wa elimu ya juu Wizara ya Elimu,Sayansi na Tekinolojia
Prof.Appolinary Kamuhabwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Afya Muhimbili(MUHAS)
……………….
Serikali imeanza kutekeleza Sera mpya ya elimu pamoja na mafunzo ambapo Sera ya mwaka 2014 ambayo imefanyiwa marejeo makubwa ikaitwa Sera ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023, Sera hiyo ilivyotoka ilishababisha mtaala kubadilishwa kuanzia ngazi za chini hadi vyuo na hivi sasa taasisi za elimu ya juu nazo kuendana na Sera hiyo.
Hayo yameelezwa na Laurence Msofe Mkurugenzi wa elimu ya juu Wizara ya Elimu,Sayansi na Tekinolojia ambaye ni mgeni Rasmi katika kongamano la mradi wa mabadiliko katika ufundishaji wa wataalamu wa Afya.
Aidha amesema kuwa mradi huo umeendeshwa takribani miaka 6 na ni mradi ambao unahusisha vyuo vya hapa Tanzania,Chuo Cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili lakini pia Chuo cha KUHAS,KCMS pamoja na vyuo viwili kutoka nje Chuo cha DUKES na Chuo cha St.Francisco university of California Marekani.
“Lengo la huu mradi ni kufanya mapitio makubwa katika namna ya kufundisha wataalamu wa Afya na lengo lake ni kupata wataalamu wa Afya ambao wana ujuzi lakini pia wanauwezo wa kutenda kazi zao kwa umahiri mkubwa”
“Mradi huu umefanikiwa kutengeneza mitaala ya mfano katika mafunzo ya udaktari,lakini pia mafunzo ya unesi na ni mitaala ambayo imeshapitishwa na taasisi yetu ya tume ya vyuo vikuu Tanzania na tunatarajia kwamba itatumika sasa sio tu kwa vyuo hivyo ambavyo nimevitaja lakini pia kwa vyuo vingine hapa Tanzania” Amesema.
Aidha ameongeza kuwa kikubwa ambacho kimepatikana kwenye mradi huo ambao umefadhiliwa kwa kiasi kikubwa ni kupata namna tofauti ya kuangalia ufundishaji katika masomo hayo ya tiba hasa kwa udaktari na uuguzi.
Kwa upande wake Prof.Gideon Kwesigabo ambaye ni mratibu wa mradi amesema mradi huo katika utekelezaji wake wamefuata njia tatu ambazo ni kubadilisha mtaala,kuomgeza uwezo wa walimu kufundisha pamoja na kuhusisha wadau kuhakikisha kwamba wadau wanahusika katika mradi huo ili vitu ambavyo wamevifanya viweze kuwa na umuhimu kwa wadau wote ambao wana shirikiana nao.
Vilevile wameweza kutengeneza watu ambao ni jumuiya ya watu waliomaliza katika vyuo vyao ambao wanaendelea kuwasiliana na kuambiana changamoto zao na wao kama walimu wanaendelea kushirikiana nao kuhakikisha mahitaji yao ya kitaaluma ambayo wanakutana na changamoto katika kazi zao yaweze kusuluhishwa.
Naye Prof.Appolinary Kamuhabwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Afya Muhimbili(MUHAS) amesema lengo la mradi ni kuangalia namna bora ya ufundishaji wanayo fundisha wataalamu wa afya na namna wanavyo watahini na vitu gani wanatakiwa kuvijua kulingana na mazingira ya Tanzania na ulimwenguni,hivyo mradi umewasaidia sana kuweza kutekeleza mitaala pamoja na wataalamu wa kufundisha.
“Huu mradi tunaona kwa kiasi kikubwa unaenda kuinua ubora wa mafunzo ya afya kwa elimu ya juu hapa nchini na tunaishukuru Wizara ya elimu kwa kulipokea vizuri na baada ya kongamano hili tutawasilisha mapendekezo” Amesisitiza