Mazingira mazuri na wezeshi yaliyopo Mkoani Lindi yavutia wawekezaji kutoka Visiwa vya Conoro kuwekeza mabilioni ya fedha katika mkoa wa Lindi
Amil Mahamoud mmoja wa wafanyabiashara wakubwa kutoka visiwa vya Anjouan – Comoro amefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kufanya mazungumzo na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi BZuwena Omary juu ya dhamiira yake ya kuanzisha kiwanda cha kujenga fiber boat za kisasa na lengo la kutumia bandari ya Lindi kusafirisha bidhaa Kwenda Anjouan.
Omary amempongeza mfanyabiashara huyo kwa lengo lake la kuchagua Mkoa wa Lindi kufanya uwekezaji wa aina hiyo kwani Lindi ni sehemu sahihi na tulivu kwa uwekezaji wowote.
Amesema Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa Mikoa yenye utajiri Mkubwa kuanzia aridhini na baharini kwani inaeneo kubwa ambalo linahitaji wawekezaji wa aina yoyote kulingana na utaratibu na vigezo.
Omary ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa viongozi na wananchi wote wa Mkoa wa Lindi kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi, kwani kufanya hivyo kutaendelea kuvutia wawekezaji wengi zaidi.
Bandari ya Lindi tayari imeanza kutumika na wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo ambao wanasafirisha Ng’ombe kutoka Lindi Tanzania kuelekea Visiwa vya Comoro kwa hali hiyo Lindi ni sehemu sahihi kwa uwekezaji.