Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpongeza Afisa Muuguzi kutoka nchini Zambia Christine Musonda aliyehitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKDI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na maafisa Uuguzi kutoa nchini Zambia waliohitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo wakati wa kuwaaga jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi kutoka nchini Zambia Erica Khunga akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa Uuguzi wanne kutoka nchini humo waliokuwa wanachukua mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpongeza Afisa Uuguzi kutoka nchini Zambia Aoraida Nkhoma aliyehitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpongeza Afisa Uuguzi kutoka nchini Zambia Able Kaunda aliyehitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wauguzi kutoka nchini Zambia waliohitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga jijini Dar es Salaam.
………………….
Na: Stella Gama – Dar es Salaam
26/08/2024 Wauguzi kutoka nchini Zambia walioudhuria mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na wa dharura wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wanaporejena nchini mwao na kutumia vizuri ujuzi walioupata wanapowahudumia wagonjwa hao.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wauguzi hao iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kisenge alisema kupitia mafunzo waliyopata kwa kipindi cha miezi sita wauguzi hao waono uwezo wa kuokoa maisha ya wagonjwa mahututi kwani wagonjwa hao wanahitaji uangalizi wa karibu zaidi.
“Kuna nchi nyingi wanatoa mafunzo kama haya, lakini nyie mmechagua kuyapata hapa kwetu Tanzania hii nikutokana na uhusiano mzuri tulionao baina ya nchi zetu hizi mbili”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema mbali na kushiriki katika mafunzo hayo wauguzi hao pia wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vilivyopo nchini ikiwa ni sehemu ya kufanya utalii na kujifunza kutoka kwetu.
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joshua Ogutu alisema kupitia mafunzo waliyopata wauguzi hao wataenda kubadilisha utoaji wa huduma na kuokoa maisha ya wagonjwa wanaowahudumia.
Ogutu ambaye pia ni Muuguzi wa JKCI alisema wauguzi hao wamepitia hatua zote za kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi pamoja na kutumia mashine zinazotumiwa na wagonjwa hao kama vile mashine ya kusaidia kupumua.
“Kupitia elimu waliyoipata hapa wagonjwa wa dharura watakaopitia katika mikono yao watakuwa salama kwani hatua zote za kuwahudumia wagonjwa mahututi zimefanyika kwa vitendo wakati wa mafunzo”, alisema Ogutu
Naye muuguzi kutoka nchini Zambia Erica Khunga aliishukuru JKCI kwakuanzisha mafunzo hayo kwani yamekuwa na umuhimu kwao kama wauguzi katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Erica alisema wataendelea kutumia fursa ya mafunzo iliyopo JKCI kuendelea kujifunza katika maeneo mengine yakutoa huduma kwa wagonjwa ikiwemo katika chumba cha upasuaji mdogo wa moyo.
“Kupitia mafunzo haya imekuwa mara yangu ya kwanza kutoa huduma katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu, nilivyokuja ni tofauti na ninavyoondoka”, alisema Erica.
Mafunzo kwa wauguzi ya kuwahudumia wagonjwa ya dharura na mahututi yaliyoanza mwezi Machi na kumalizika mwezi Agosti 2024 yanakuwa mafunzo yakwanza kumalizika JKCI ikiwa inashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).