Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo wakati alipohani msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi Waziri Mkuu alitoa pole kwa Niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Wanafamilia, ndugu, jamaa na waombolezaji wote kutokana na msiba huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………….
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 24, 2024 amehani msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi.
Akizungumza kwa Niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa, Rais Dkt. Samia anatoa pole kwa Wanafamilia, ndugu, jamaa na waombolezaji wote kutokana na msiba huo.
“Rais Dkt. Samia anatoa rai kwa waombolezaji wote kuendelea kuiombea familia hii katika kipindi hiki cha huzuni”.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi Agosti 24, 2024. Waziri Mkuu alitoa pole kwa Niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Wanafamilia, ndugu, jamaa na waombolezaji wote kutokana na msiba huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pole Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, kwenye msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mkewe, Nachingwea mkoani Lindi Agosti 24, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, kwenye msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mkewe, Nachingwea mkoani Lindi Agosti 24, 2024. Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa heshima za ya mwisho kwenye msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi Agosti 24, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)