Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limeendelea kufikia Makundi mbalimbali katika Jamii lengo likiwa ni kuwajengea uwezo na uelewa wa matukio ya uhalifu na ukatili unaofanywa na baadhi ya watu wasio na maadili Mkoani humo huku Jeshi likisisitiza uangalizi wa watoto.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Namagana Mkoa wa Mwanza Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Irene Mayunga wakati akitoa elimu hiyo katika kanisa la Mtakatifu Nicholas Annglikana Nyamagana ambapo ametoa elimu ya namna ya vitendo vya ukatili namna ya kuripoti matukio hayo sehemu husika likiwemo dawati hilo wilaya ya yamagana.
Ameongeza kuwa vitendo vya ukatili vikifumbiwa macho matokeo yake ni mabaya ambapo amewataka viongozi wa dini kuendelea kuvikemea katika nyumba za ibada ili matukio hayo yawe historia katika wilaya ya Nyamagana.
Sambamba na hilo ameendelea kusisitiza suala la uangalizi wa kundi la watoto ambapo amesema endapo uangalizi wa watoto utakuwa mzuri vitendo vya kupotea kwa watoto wao havitokuwepo.