Kampeni ya “Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15” ilianza Juni 10, 2024 na itaendeshwa kwa miezi 3 na wateja wengine wenye bahati wataweza kujishindia simu janja za kisasa aina ya I-phone 15. Ili kushiriki kampeni wateja wa Bank of Africa, wanatakiwa kufanya miamala ya kidigitali kupitia programu ya Benki ya simu ya kiganjani (B-Mobile) au kwa kupiga (*150*13#) kufanya miamala mingi iwezekanavyo na kutoa pesa kupitia WAKALA wa BOA ili kuingia kwenye droo inayofanyika kila mwezi.
Akiongea wakati wa droo hiyo,Mratibu wa bidhaa na huduma za kidigitali wa Bank of Africa, Bw Fortunatus Joachim, alisema kampeni hii imelenga kuwezesha wateja wa Benki kutumia mfumo wa kidigitali kupata huduma za kibenki ambao umeboreshwa kutumia simu ya kiganjani kukidhi mahitaji yao.
“Kama benki tumedhamiria kutoa bidhaa na huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja. Benki itaendelea kukuza na kuleta mawazo mapya ya ubunifu kwendana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya kidigitali katika tasnia ya benki kwa ajili ya kukuza zaidi ajenda jumuishi ya kifedha,” alisema Bw.Fortunatus.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko, Nandi Mwiyombella, alisema : “Kupitia kampeni hii, wateja wetu na wapya wanaotumia huduma za benki mtandao (Mobile Banking) wataingia katika droo iwapo watafanya miamala kwa njia ya kidigitali na kutoa fedha angalau mara moja kutoka BOA WAKALA.
Kampeni hii ni kielelezo cha lengo la kimkakati la benki kuweka bidhaa na huduma zake katika mfumo wa kidijitali na hivyo kukuza ushirikishwaji wa kifedha pamoja na urahisi wa wateja kupata huduma za benki.