Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan leo August 22,2024 ameweka Jiwe la Msingi la mradi wa Ujenzi wa Suluhu Sports Academy iliyojengwa na wadau wa Maendeleo wakiongozwa na CRDB Foundation ambapo ndani yake kutakuwa Viwanja vya Michezo mbalimbali ikiwemo Uwanja wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukuwa Watazamaji 20,000.
Awamu ya kwanza ya Ujenzi wa academy hiyo inatarajiwa kukamilika Mwezi April mwakani.
Uwekaji wa Jiwe la Msingi ni sehemu ya Shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi festival 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Suluhu Sports Academy katika eneo la Kizimkazi wakati wa shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi, Zanzibar tarehe 22 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Watoto wa Suluhu Sports Academy wakiimba mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi, Kizimkazi Zanzibar tarehe 22 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Suluhu Sports Academy katika eneo la Kizimkazi, Zanzibar tarehe 22 Agosti, 2024.