Na Prisca Libaga , Arusha
SERIKALI imewataka wajasiriamali Wanawake kupitia Vikundi vyao vya ujasirimali wanajisali kwenye mfumo ili waweze kuwezeshwa kiuchumi na hivyo kuondokana na umasikini.
Hayo yameelezwa jana Agosti 20 na Mshauri wa Rais Samia, kwenye maswala ya Wanawake na Vijana na makundi maalumu , Sophia Mjema, alipokuwa akizindua Baraza la Mkoa wa Arusha la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika ngazi ya Mkoa kwenye hafla iliyofanyika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Amesema kuwa mwaka 2027 Dkt Samia akiwa ni Makamu wa Rais alianzisha majukwaa ya Wanawake ya kiuchumi nchi nzima , mengine yanaendelea,mengine yamekufa, mengine yamelegalega na sasa amewatuma nchi nzima kuyatambua majukwaa yote katika mikoa , Wilaya na kata
Amesema kuwa Programu ya uimarishaji uchumi na mama Samia maarufu ( IMASA ) inawataka kujisajili kwenye mfumo ili kuyafikia makundi yote ya kijamii na hakuna na Mwananchi atakae achwa lengo ni kuhakikisha kila mmoja amesajiliwa kwenye mfumo huo kuanzia mitaa Vitongoji kata na kila Mkoa utapewa Programu kulingana na mahitaji yake ya kiuchumi.
Mjema, amesema ndoto ya Rais ni kuwanyanyua Wananchi wote Kiuchumi na hivyo kupitia jukwaa hilo Wanawake wanaweza kufikia uchumi wa kati,akawataka wachangamkie fursa mbalimbali za Kiuchumi zikiwemo za kitalii .
Amesema Arusha ni Mkoa wa kumi na moja ambapo wanapita kuyatambua majukwaa hayo ya Wanawake ya kiuchumi kama yapo na yanafanya kazi na kama yana watu wangapi ili Serikali ikianza kuwawezesha walioko kwenye Vikundi ifahamu inawezesha watu wenye uhutaji upi.
Amesema kuwa Programu ya Uwezeshaji wa Wanawake ,Vijana,wazee, wenye mahitaji maalumu inatekelezwa kupitia Ofisi ya mkuu wa mkoa na sarikali za mitaa
Mjema,amesema amekuja kukutana na Viongozi wa Vikundi vya wajasiriamali wa Mkoa wa Arusha ili kufahamu mahitaji yao kwenye uchumi,masoko na biashara na kuhimiza wahakikishe wanasajiliwa kwenye mfumo wa Serikali.
Amewahakikishia kwamba katika kutekeleza Programu hizo hakuna utapeli utakaotokea na ndio sababu wamekuja kuzindua baraza hilo ambalo litakuwa na Wadau mbalimbali zikiwemo benki .
Amesisitiza umuhimu wakutunza kumbukumbu ambazo zinawasaidia kufahamu hasara na faida aliyoipata mjasiriamali katika kipindi cha kuanza shughuli zake,wasipofanya hivyo watapotea kwenye biashara,pia amewataka wajitambue waache kufanya kazi kwa mazoea.
Kwa upanda wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa, amesema kazi yao kubwa ni kuwezesha Wanawake Kiuchumi ifikapo mwaka 2026 wanataka kuona mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia majukwaa ya mikoa na wilaya.
Amesisitiza kwamba kila mmoja lazima aingizwe kwenye kanzidata ndani ya mwezi mmoja na hivyo
kuwawezesha kuwanyanyua Kiuchumi.
Amesema wamekuja Arusha kujua Wananchi kuwa wanahitaji nini kama ni mafunzo,mitaji ,mashine, au vifaa ikiwemo mbolea na masoko.
Beng’i, amesema programu ya uimarisha uchumi na mama Samia inawataka kutambua kuwa mafanikio yao ya kiuchumi yanawategemea wenyewe na Baraza ni kuwawezesha tu.
Amesema kuwa Mkoa wa Arusha utawasilisha vipaumbele kwenye Baraza hilo la taifa ndani ya wiki moja ili Baraza liweze kuandaa programu ambayo itawawezesha Wanawake kuinuka Kiuchumi.
Amewataka wajasiriamali hao kujitambua na kujipanga Kwa kuwa biashara inataka umakini ,kujua muda na masoko na wateja hivyo lazima kila mmoja awe na malengo